'Wachana na ex,'Mashabiki wamwambia Miracle baby baada ya kumuomba mkewe arudi nyumbani

Muhtasari
  • Baadhi ya mashabiki wake walimwambia msanii huyo awache kusumbuana na ex wake na aweze kuendelea na maisha yake
  • Katika chapisho lililoshirikiwa kwenye Instagram, msanii wa Gengetone anamwomba mkewe arejee nyumbani

Uhusiano kati ya msanii wa gengetone Miracle Baby na mkewe hauyuko vyema kama inavyodhaniwa kwani,kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemsihi arudi nyumbani.

Baadhi ya mashabiki wake walimwambia msanii huyo awache kusumbuana na ex wake na aweze kuendelea na maisha yake.

Katika chapisho lililoshirikiwa kwenye Instagram, msanii wa Gengetone anamwomba mkewe arejee nyumbani.

Anaenda mbele kuomboleza jinsi mkewe alivyomnyima muda na marafiki zake na hata jinsi anavyomkaripia kama mtoto mchanga kila anapofanya jambo baya.

"Nitaongea ukweli umenikalia saana saaana umenifungia saana ady sipati time na maarif wangu nikidu kitu ya ufala wewe hunikelelesha Kama mtoto mdogo."

Mwimbaji mkuu wa Sailors alitaja kwamba licha ya hayo yote hajapata mtu yeyote anayemtendea jinsi mpenzi wake anavyofanya.

"lakini wacha nikuambie kitu moooja na uniskize kwa makini siku yenye utawai badilisha kuduu ivo wee hunidu tutakosana na nitakusema kwa mum coz nmezunguka Dunia sijawai pata mwenye atanipatia favor yenye umenipea beb nakupenda coz you are two in one una represent my mum na my wife at the same time I love you and am missing you rudi nyumbani toto...💍."

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

game_changers254: Budaa warembo ni kibao. Wachana na ma ex kujia ma why🔥🔥🔥🔥

dj_madkev254: Real men are loyal and supportive happy life ahead😍 😍🔥🔥

terry.murigi: Wow😍 just wow those words ,i love when people love each other ,may this love live forever❤️Katrue ebu Rudi home

pinky.betty: 😂😂ako wapi aty unakeleleshwa