Msanii Wilson Abubakar Radido almaarufu Willy Pozee amelezea kukerwa na wanamitandao wanaomuita Bwana Mkunaji.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha video akiwaeleza mashabiki wake kwamba mwaka huu mpya anawaomba waache kumwita jina hilo.
"Tafadhali, watu wangu, acheni kuniita bwana mkunaji. sitaki kuitwa bwana mkunaji kwa sababu mnazuia baraka za wimbo mpya wa toto kutambulika," Willy alieleza.
Hivi majuzi Willy Paul alitoa taarifa akieleza maana fiche ya mkunaji.
,'Mkunaji' ni jina ambalo linahusishwa na mambo mabaya na kudai matatizo mengi yamekuwa yakimkumba kutokana na jina hilo.
"Ninapenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha wote kuwa kuanzia leo sitakuwa natumia jina la 'MKUNAJI', ni baya na sitaki kujihusha nalo! Tangu nilipokubali jina hilo nimekuwa na matatizo mengi sana"alisema Pozee.
Kulingana naye wimbo ambao ametoa mwaka huu haufanyi vizuri kwa sababu ya itikadi za jina ambalo mashabiki wake walimbandika.