logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rufftone kuwania useneta wa Nairobi kwa UDA

Ruffton alisema mwaka 2007 baada ya uchaguzi mkuu, ndugu yake Daddy Owen, ambaye pia ni mwanamuziki tajika wa nyimbo za injili alimfurusha nyumbani kwa upanga,  baada ya kutofautiana vikali kuhusu siasa za mirengo pinzani wakati huo.

image
na

Yanayojiri26 January 2022 - 06:14

Muhtasari


• Amezungumza mengi kuhusu azma yake na sababu kuu kuingia mrengo wa naibu Rais William Ruto na si ODM kama wengi wa wafuasi wake walivyokuwa wakitarajia.

• Ruffton anafahamika sana kwa wimbo wa injili kwa jina 'Mungu Baba', kibao ambacho aliwashirikisha polisi kutoka kitengo cha GSU takribani miaka minane iliyopita.

RUFFTONE

Mwanamuziki wa injili Smith Mwatia almaarufu Ruffton na ambaye ana azma ya kuwa seneta wa Nairobi ametangaza kwamba atagombea kiti hicho kwa tiketi ya UDA.

Amezungumza mengi kuhusu azma yake na sababu kuu kuingia mrengo wa naibu Rais William Ruto na si ODM kama wengi wa wafuasi wake walivyokuwa wakitarajia.

Ruffton anafahamika sana kwa wimbo wa injili kwa jina 'Mungu Baba', kibao ambacho aliwashirikisha polisi kutoka kitengo cha GSU takribani miaka minane iliyopita.

Mwanamuziki huyo anadai kuwa uamuzi wake kujiunga na mrengo wa naibu rais unatokana na madai kuwa chama cha ODM kinahusishwa pakubwa na wahuni wapenda vurugu na ndio sababu kuu imemfanya kuingia UDA.

Akitoa mfano, Ruffton alisema mwaka 2007 baada ya uchaguzi mkuu, ndugu yake Daddy Owen, ambaye pia ni mwanamuziki tajika wa nyimbo za injili alimfurusha nyumbani kwa upanga,  baada ya kutofautiana vikali kuhusu siasa za mirengo pinzani wakati huo.

Ruffton anasema kipindi hicho yeye alikuwa mfuasi wa chama cha PNU ambacho ni cha  rais mstaafu Mwai Kibaki ilhali ndugu yake Daddy Owen alikuwa ni mfuasi sugu wa chama cha ODM.

Kisa hicho cha Owen kumfukuza Ruffton kwa panga kilimpelekea kuchukia chama cha ODM na hata kukihusisha na vurugu za uchaguzi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved