Baraza la Sanaa Nchini Tanzania, BASATA latarajia kukuwakutanisha wasanii sifika wa nchi hio kwenye uzinduzi anaofanyika tarehe 28 Januari 2022.
Baraza hilo ambalo limekuwa limesitisha tuzo hizo kwa muda,lilitangaza kupitia ukurasa wake wa instagram kwamba wanarudisha tuzo hizo.
Kulingana nao, tuzo hizo zitashirikisha wasanii kutoka ndani ya nchi pekeeTanzania.
Wasanii ambao wamepokea mwaliko rasmi ni;Alikiba, Diamond, Harmonize,Nandy, Zuchu na miongoni mwa wengine.
Alikiba anatarajiwa kukaa meza moja na Diamond jambo ambalo si la kawaida kwani wasanii hao wawili hawajawai kutana kwenye tamasha yoyote.
Isitoshe, itakuwa mara ya kwanza Diamond kukutana na Harmonize baada ya kugura Lebo yake ya WCB na kutengeneza Lebo yake mpya.
Harmonize mwezi jana alipokuwa akirejea nchini Tanzania, alieleza yote yaliyomkumba wakati alikuwa akifanya kazi na Lebo ya Diamond.
Kilichoshangaza zaidi kwenye mialiko hio , Diamond na Zuchu ndio wamepokea mwaliko rasmi kutoka timu wasafi.