Jacque Maribe azungumza baada ya kufumaniwa na mpenzi mpya

Muhtasari

•Jacque Maribe kuonekana  kwenye mtandao akiwa anapiga busu hadharani  jamaa aliyekadiliwa kuwa mpenzi wake mpya

•Inasekama kuwa Maribe alikuwa kwenye Klabu moja mjini Nyeri, ambapo alikuwa na mwanaume aliyemtambulisha kama rafiki yake kwa marafiki zake

Jacque Maribe
Jacque Maribe
Image: hisani

Mwanahabari Jacque Maribe tena amekuwa gumzo mtaani baada kuonekana  kwenye mtandao akiwa anampiga busu hadharani  jamaa aliyedhaniwa kuwa mpenzi wake mpya.

Inasekama Maribe alikuwa kwenye Klabu moja mjini Nyeri, ambapo alikuwa na mwanamume aliyemtambulisha kama rafiki yake.

Kutokana na kuenezwa kwa picha hio  kwenye mitandao ya Kijamii Jacque amejitokeza kupitia ukurusa wake wa Insta stories  na kuwaeleza wanamitandao kuwa walichokuwa wanadhani wanakijua sio hivyo bado wamo katika giza totoro, hawajui lolote kumhusu.

"Character development day is here..Wanapofikiri wanajua, hawajui- methali ya mtu" alisema Maribe.

Aliendeleza kueleza ameamua kuja na mbinu mpya ya kuwachanganya madui wake ili wasipate la kuongea.

"Wachanganye maadui kwa gharama yoyote." alisema Jacque kuwajibu walio kuwa wakieneza habari hizo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Jacque kuhusishwa na mtu,  baada ya uhusiano wake na Jowie Irungu kusambaratika.