Mama Diamond asifia aliyekuwa mpenzi wa mwanawe, Wema Sepetu

Muhtasari

•Ingawa kumekuwa na tetesi kwamba Diamond anatoka kimapenzi na msanii Zuchu huku uvumi huo ukiwavutia wengi na kutaka kujua kama ni kweli  wasanii hao wanachumbiana

•Mama Dangote ameonekana kuwa na mtanzamo tofauti huku siku Jumatanne alichapisha video kwenye ukurasa wake wa Instagram ambako aliionekana akiwa amevalia dera alilonunuliwa na Wema Sepetu.

mama dangote
mama dangote
Image: hisani

Mamake Diamond, Sanura Kasimu almaarufu Mama Dangote amesifia aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Mwanawe, Wema Sepetu.

Ingawa kumekuwa na tetesi kwamba Diamond anatoka kimapenzi na msanii Zuchu huku uvumi huo ukiwavutia wengi na kutaka kujua kama ni kweli wasanii hao wanachumbiana. 

Mama Dangote ameonekana kuwa na mtanzamo tofauti na siku Jumanne alipakia video kwenye ukurasa wake wa Instagram ambako aliionekana akiwa amevalia dera alilonunuliwa na Wema Sepetu.

 Kulingana naye, vazi hilo alinunuliwa na Wema Sepetu siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake na inabaki kama kumbukizi maishani.

Mashabiki  wa wasanii hao wamebaki njia panda wakishindwa kwa nini Mama Dangote anaonekana kuwa hazungumzii mahusiano ya mwanawe na Zuchu ilhali Mama wa Zuchu alizungumza kuhusu habari za mwanawe na Diamond.