Msanii wa nyimbo za injili Daddy Owen amesema kwamba msanii Rufftone alimuomba msamaha baada ya matamshi yake akiwa kwenye mahojiano.
Owen akiwa kwenye mahojiano ya kipekee na Mpasho, hajawahi mbebea ndugu yake panga kama ilivyosemekana kwenye mahojiano.
"Aliniomba msamaha jana, alisema kuwa yalikuwa makosa."
Daddy Owen alieleza kwamba Rufftone alitamka maneno hayo, ilhali kwa maana halisi alimaanisha kuyatumia kama kielelezo.
“Pia nilishtuka, tulikuwa na kikao cha familia jana, tukajadiliana, akakiri kuwa amekosea, akakiri kuwa anataka kutumia chochote atakachosema kuwa kielelezo cha jinsi watu wanavyoweza kupenda siasa lakini ikatoka vibaya. Anasema alitumia kielelezo kibaya kuweka hoja,” Daddy Owen alisema.
Owen alisema kuwa Rufftone- ambaye ni mpya katika ulingo wa kisiasa alieleweka vibaya na watazamaji.
"Watu hawakumwelewa. Tulikutana jana...nikamuuliza nini kilitokea. Akasema bado yuko fresh kwenye ulingo wa siasa, kuna wakati anajikuta anajirekebisha."
Rufftne akiwa kwenye mahojiano na NTV Alipoulizwa ni nini kuhusu ODM ambacho hakihusiani naye vyema, Rufftone alisema, "kuna vuguvugu la uhuni."
"Niliamini kuwa siasa ni itikadi, na tukiachana na wewe kisiasa, huna haja ya kunidhuru, iwe kwa maneno au kimwili," alisema.