Zuchu Tayari amelipiwa mahari

Muhtasari

•Tetesi za mahusiano baina ya wanamuziki hao zimefanya Mama wa Zuchu, Bi Khadija Kopa wiki jana kujitokeza na kuzungumzia mahusiano ya mwanawe na Diamond

•Zuchu alisainiwa  kwenye Lebo hiyo, siku ya Aprili  8, 2020, ambapo amekuwa akitoa ngoma sifika za Bongo. 

•Kauli hiyo ya Bi Khadija iliwandia baada ya zuchu kuthibitisha kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu aliyempatia zawadi ya mdoli ya mdoli mkubwa

Khadija Kopa, Zuchu
Khadija Kopa, Zuchu
Image: HISANI

 Habari za Zuchu  na Diamond Platnumz  zimekuwa zikienea kwa kasi, si kwa vyombo habari, si kwa mtandao wanablogu hawajasazwa.

Tetesi za mahusiano baina ya wanamuziki hao zimefanya Mamake Zuchu, Bi Khadija Kopa wiki jana kujitokeza na kuzungumzia mahusiano ya mwanawe na Diamond.

Zuchu alisajiliwa kwenye Lebo ya Wasafi,  Aprili  8, 2020, ambapo amekuwa akitamba kwa ngoma kali za Bongo kama vile Sukari, Mwambieni, Nyumba ndogo miongoni mwa vibao vingine. 

Wawili hao wamekuwa na ukaribu wenye  viulizo si haba hasa baada ya kunaswa hotelini  wakiwa wanaburudika pamoja mwezi uliopita.

Bi Khadija alisema mwanawe amelipiwa mahari bila kutaja mtu aliyemlipia.

Kauli hiyo ya Bi Khadija iliwadia baada ya zuchu kuthibitisha kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu aliyempatia zawadi ya mdoli ya mdoli mkubwa. 

“Mimi sina taarifa kwamba anaolewa na Diamond, lakini ninachojua tayari zuchu amelipiwa mahari…”Bi khadija alisema.