Chris Brown atuhumiwa kulewesha na kumbaka mwanamke katika boti la kifahari

Muhtasari

•Kisa hicho kinadaiwa kutokea kwenye mashua ya kifahari mnamo Desemba 30 mwaka 2020 huko Miami, Florida.

•Mwanamke huyo anadai kuwa alipewa vinywaji na Brown baada ya kuwasili, na baadaye akahisi "badiliko la ghafla, lisiloelezekala ufahamu".

Image: GETTY IMAGES

Chris Brown ameshtakiwa kwa kumlewesha na kumbaka mwanamke mmoja na sasa anadaiwa dola milioni 20.

Kisa hicho kinadaiwa kutokea kwenye mashua ya kifahari mnamo Desemba 30 mwaka 2020 huko Miami, Florida.

Radio 1 Newsbeat imewasiliana na mameneja wa Chris Brown kutoa maoni yao lakini bado hawajajibu.

Chris Brown ameonekana kujibu kwenye akaunti yake ya Instagram, akidai kuwa anashitakiwa kwa sababu anatoa muziki mpya.

Kesi hiyo imewasilishwa na mcheza densi na mwanamuziki ambaye hakutambulika, ambaye ametajwa tu kama 'Jane Doe' katika nyaraka za mahakama.

Hati hizo zinaangazia madai matano tofauti dhidi ya mwimbaji huyo yakiemo unyanyasaji wa kijinsia, na ukiukaji wa Sheria ya Unyanyasaji wa Kijinsia.

Mwanamke huyo anadai "anahofia maisha na kazi yake".

Anasema alialikwa kwenye meli na rapa na produsa Diddy, ambapo kisa hicho kinadaiwa kilifa

Mwathiriwa anasema kwamba alichanganyikiwa alipopewa kinywaji na Chris Brown
Mwathiriwa anasema kwamba alichanganyikiwa alipopewa kinywaji na Chris Brown
Image: GETTY IMAGES

Kulingana na nyaraka moja, mwanamke huyo anadai kuwa alipewa vinywaji na Brown baada ya kuwasili, na baadaye akahisi "badiliko la ghafla, lisiloelezekala ufahamu".

Nyaraka hiyo inadai kuwa "alichanganyikiwa na akaanza kuhusi usingizini", kabla ya kupelekwa hadi chumbani ambako Brown anadaiwa kumvua nguo na kumbaka.

Inasemekana Brown aliwasiliana na mwanamke huyo siku iliyofuata, na kumwambia akunywe vidonge vya kuzuia ujauzito.

Kitengo cha Newsbeat pia kimejaribu kuwasiliana na wawakilishi wa Diddy, lakini bado haijapokea jibu.