(+Picha) Mhubiri Lucy Natasha na Prophet Carmel wafunga pingu za maisha katika harusi ya kitamaduni

Muhtasari

•Prophet Carmel ambaye ana asili ya Kihindi alimvisha Natasha pete ya uchumba mnamo mwezi Novemba mwaka jana.

Mhubiri Lucy Natasha aolewa katika harusi ya kitamaduni
Mhubiri Lucy Natasha aolewa katika harusi ya kitamaduni
Image: FACEBOOK// LUCY NATASHA

Mhubiri mashuhuri nchini Lucy Natasha na kipenzi chake Prophet Carmel kwa sasa ni mke na mume kirasmi baada yao kufunga pingu za maisha katika harusi ya kitamaduni iliyoandaliwa Jumamosi.

Wawili hao ambao wamekuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kisichothibitishwa walipiga hatua hiyo muhimu maishani mbele ya familia na marafiki wachache waliokuwa wamealikwa.

Natasha alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutangazia wafuasi wake kuhusu harusi yake huku akieleza ilikuwa siku ya kukata na shoka.

"'Mapenzi ni kitu kitamu, unapopata mwenzako bora, siku zako hujawa na furaha, furaha na utimilifu. Nyakati za furaha wakati wa Harusi yetu ya Kitamaduni." Natasha aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Prophet Carmel ambaye ana asili ya Kihindi alimvisha Natasha pete ya uchumba mnamo mwezi Novemba mwaka jana.

Mamia ya Wakenya wamejumuika mitandaoni kuwapongeza wawili hao wanapojiandaa kuanzisha familia pamoja.