logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mambo ni shwari kati ya Rayvanny na mpenziwe Paula Kajala

Paula kajala ambaye ni mtoto wa muigizaji maarufu Tanzania Kajala Masanja.Wiki jana, wapenzi hao waliachana kufuatiliana kwenye ukurasa wao huku huku Paula akifuta picha alichokuwa amechapisha kwenye ukurusa wake wake wa Instagram.

image
na

Habari31 January 2022 - 05:01

Muhtasari


•Paula kajala ambaye ni mtoto wa muigizaji maarufu Tanzania Kajala Masanja.Wiki jana, wapenzi hao waliachana kufuatiliana kwenye ukurasa wao huku Paula akifuta picha alichokuwa amechapisha kwenye ukurusa  wake wa Instagram

•Ikumbukwe Baba Levo alijitokeza Jumanne na kueleza kwamba alimuonya Ravyaan kuhusu kulipia mpenzi wake karo,  akisema mpenzi hasomeshwi kwa sababu akipata elimu kukuzidi  atakutoroka.

 Baada ya staa wa Bongo flavor Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny kuacha kufuata mpenzi wake Paula Kajala kwenye ukurusa wa Instagram, tetesi ziliibuka kwamba wapenzi hao wamechana.

Wiki jana Paula Kajala ambaye ni mtoto wa muigizaji maarufu Tanzania Kajala Masanja na Rayvanny waliacha kufuatana kwenye mtandao wa Instagram huku mlimbwende huyo  akifuta picha alizokuwa amepakia.

Sasa imebainika wawili hao wamerudi kufuatana  baada ya wiki moja ya tetesi kuwa wameachana kuenea mitandaoni.

Kulingana na  kitendo cha kurejea kufuatilia kwenye mitandao ni bayana wazi kuwa hali mambo yako shwari kati yao.

Ikumbukwe Baba Levo alijitokeza Jumanne na kueleza kwamba alimuonya Ravyaan kuhusu kulipia mpenzi wake karo,  akisema mpenzi hasomeshwi kwani akipata elimu kukuzidi  atakutoroka.

Haya yamejiri siku chache baada ya Fayvaan ambaye ni Baby mama wa Ravyaan kusema ikiwa mwanamitindo Kim Kardashian waliachana na Rapa wa Marekani Kanye West sembuse wao.

Alisema hayo wakati alipokuwa akijibu shabiki moja aliyemwambia  aliyemliza kwa nini huwa hataki kuacha Ravyaan.

Kinachusibiriwa  sasa nikuona  kama wapenzi hao watachapicha picha pamoja na kuandikiana jumbe tamu za mapenzi kama ilivyo ada yao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved