Msanii wa Tanzania Nandy almaarufu The African Princess amejitokeza na kuwauliza mashabiki wake wamshauri kuhusu msanii wa kwanza ambaye wangependa afanye naye collabo.
Kupitia ukurusa wake wa Instagram, Nandy ametoa orodha ya wasanii ambao anatarajia kuingia nao studio kuandaa muziki huku akitaka mashabiki wamshauri ni Collabo gani wangetaka kusikia kwanza.
Baadhi ya wasanii aliowataja kwenye orodha hiyo ni; Sauti Sol, Patoranking, Davido na dulamakabila.
Vilevile, ameeleza kuwa collabo hizo ziko tayari kilichosubiriwa ni mashabiki kusema wimbo gani wanataka awapakulie mwaka mpya.
Nandy ambaye pia ni muigizaji wa filamu Tanzania, amekisiwa kwamba mwaka huu wa 2022atafunga ndoa siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi mwaka huu 2022 lazima atafunga ndoa na mpenzi wake Bilnass.
Jumatatu, msanii huyo alitangaza kuwa anaendelea na vikao vya kupanga mikakati ya tamasha lake ambalo linatabiriwa kufanyika kabla mwezi wa nne ,huku mipango kabambe ikishika kasi kuhakikisha kila kitu kinashughulikiwa kabla ya tarehe rasmi.