Wema Sepetu amfikisha mahakamani Aristostle kwa matamshi ya udhalilishaji

Muhtasari

•Mwanasheria wa Wema Sepetu ameeleza kwamba wameenda makamani kuhakikisha mteja wake amepata kulipwa  kutokana na maneno yaliyotolewa na Aristostle.

• Aristostle kisu chake kimotoni baada ya maneno aliyoyatoa kuhusu muigiaji maruufu nchini Tanzania  Wema Ssepetu, ambayo yalichukuliwa kama kudhalilisha jinsia ya  kike kwa jumla.

wema 5 (1)
wema 5 (1)
Image: HISANI

Ni bayana sasa mwanahabari na mwandani wa Irene Uwoya , Aristostle kisu chake ki motoni baada ya maneno aliyoyatoa kuhusu muigiaji maruufu nchini Tanzania  Wema Ssepetu, ambayo yalichukuliwa kama udhalilishaji wa jinsia ya  kike kwa ujumla.

Wema Sepetu amemfikisha Aristostle  mahakamani baada ya kushauriana na wakili wake kuhusu matamshi ya mwanahabari huyo.

Kupitia kituo kimoja cha  radio nchini humo, wakili wa Wema Sepetu ameeleza kwamba wameenda makamani kuhakikisha mwigizaji huyo amepata kulipwa  kutokana na maneno ya udhalilishaji  yaliyotolewa na Aristostle.

Ikumbukwe Aristostle  alionyesha kujuta maneno yake na akajitokeza kumuomba msamaha muigizaji huyo. Msamaha wa mwanahabari huyo unaonekana kugonga ukuta, huku mwanasheria wa Wema akiwa ashamfungulia kesi mwanahabari huyo.

"Tunafuatilia kuona kwamba msanii wangu amepata kulipwa. kwa sababu ametukanwa, na watu walio na pesa, Irene ana pesa  natumai atamsimamia Aristotle na yeye amlipe mteja wangu. Msamaha aliyeomba Aristotle hufai kamwe kuitwa msamaha kwa sababu alijua vyema alichokuwa akitenda," alisema mwanasheria wa Wema Sepetu.

Kutokana na cheche za maneno na matusi ya mashabiki  yaliyotawala  ukurusu wa Aristostle imemlazimu kuchokonoa ukurusa wake wa instagram.

Ni kweli wazi kuwa chochote usemacho  kuhusu mtu mwingine kufikiria kabla ya kutenda usije ukajichimbia kaburi yako mwenyewe.