Rapa Drake ameacha kuwafuatialia Rihanna na A$ap kwa Instagram ambao walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza mwaka huu 2022.
Drake ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa Rihanna ame - unfollow wapenzi hao huku wanamitandao wakianza tetesi kwamba amekerwa na Rihanna kuwa na mimba ya A$ap.
Jumatatu Rihanna na mpenzi wake walitangaza hadharani kuwa wanatarajia kifungua mimba wao na kuonekana wakiwa na furaha isiyokifani.
Habari hizo za ujauzito wa Rihanna zilizogonga vichwa vya habari kwenye majukwaa yote ya habari.
Habari za Rihanna zimetrendi kwa siku tatu mtawalia pale twitter.
Rihanna ni msanii wa kike anayefuatiliwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na pia ngoma zake zinasikizwa dunia kote.