Ombi langu lililojibiwa-Muigizaji Mama Baha afichua jinsi alivyopatana na mumewe

Muhtasari
  • Mwigizaji Mama Baha afichua  jinsi alivyopatana na mumewe
Mama-Baha-Wanjiku-Mburu (1) (1) (1) (1)
Mama-Baha-Wanjiku-Mburu (1) (1) (1) (1)

Aliyekuwa mwigizaji wa kipindi cha Machachari Wanjiku MBuru almaarufu kwa jina lake la uigizaji kama Mama Baha, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua jinsi alivyo patana na mpenzi wake.

Alifichua hayo alipokuwa akisherehekea na kuadhimisha mwaka mmoja  kwenye uhusiano wao.

Kwa sasa mwigizaji huyo anatarajia mtoto wake wa kwanza.

Aliongeza kuwa mume wake David ni sala iliyojibiwa baada ya maombi ya siku tano na kufunga mnamo 2018.

Alisema moja ya vitu alivyoombea ni mume na Mungu alijibu maombi yake mnamo 2021.

"Ombi langu lililojibiwa @davidkinyast Februari 2018 nilienda kwa maombi ya siku tano na kufunga na moja ya maombi yangu ilikuwa mume (tunapaswa kuwa na makusudi juu ya hili), niliomba kwa mtu anayemcha Mungu, mtu kutoka kwa ghala yake mwenyewe, ambaye aliniwekea mimi.

Kufikia mwisho wa maombi na kufunga, Mungu alizungumza nami na kusema atanipa mume na hivyo nikarudi nyumbani nikimtarajia Bwana.

Songa mbele hadi Februari 2, 2021 Mungu alijibu maombi yangu kwenye kile kilima cha Ngong.

Imekuwa mwaka mmoja tayari mpenzi wangu na ninachoweza kusema ni kwamba ninamshukuru Bwana kwa ajili yako! HAPPY ANNIVERSARY WAMINE!"