Miss P asema anatamani kukutana na Otile Brown

Muhtasari

•Miss P  amefunguka na kueleza nia yake ya  kutaka kukutana na msanii sifika humu nchini Otile Brown

•Katika mahojiano na kipindi kimoja cha habari   ameeleza  kwamba mwanamuziki anayependa kusikiza kazi zake na angetamani sana kukutana naye angalau wazungumze ni Otile

Miss P
Miss P
Image: instagram/miss p

Msanii  wa kike  Miss Picasah almaarufu Miss P  ameelezea nia yake ya  kutaka kukutana na msanii sifika humu nchini Otile Brown.

Katika mahojiano na kipindi kimoja  alisema kwamba anapenda kusikiza kazi zake Otile na angetamani sana kukutana naye angalau wazungumze.

"Natamani nikutane na Otile Brown kwa sababu naona tunawiana kitabia, ananipa hamu ya kutamani sana kumuoana," alisema Miss p.

Miss P  ni msanii chipukizi ambaye alijulikana wakati alitangaza kuondoka kwa lebo ya Saldido ya Willy Paul.

Baadhi ya nyimbo za Miss P ni; Baby shower, single, Liar na Mashallah.

Aidha alisisitiza kwamba kamwe hawezi kurudi kufanya kazi yoyote na msanii Willy Paul, ikifahamika kwamba Miss P alikuwa chini ya Saldido Record ila baadaye wakatengana.