Mwanamuziki, Mercy Masika amewarai vijana ambao bado hawajafunga ndoa kujitenga na ngoma ya ndoa hadi watakapo ingia katika ndoa.
Kupitia video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwashauri vijana kuwa ni vyema vizuri kuepukana na tendo la unyumba na ilhali hawako tayari kuanza familia.
Alieleza vijana kuwa popote watapokuwa wakitembea watakutana na watu wanaovutia zaidi hivyo basi hio isiwe ni kizingizio cha kujamiana kiholela.
"Siku zote utapata watu wa kuvutia popote uendapo iwe umeoa au hujaolewa. Watu wa kuvutia watakuwepo kila wakati," alisema Mercy masika.
Isitoshe, alizungumza kuhusu wanandoa ambapo aliwashauri kuwa wajasiri na wavumilivu kwenye ndoa kwani anaelewa vyema ndoa sio jambo rahisi hasa wakati huu wa karne ya ishirini na moja.
"Kuwa hodari na jasiri kwenye ndoa ni kukubali kuwa wewe ni mzuri...kuwa hodari katika maisha kama Mungu anavyotaka kutoka kwako," alieleza.