Mpenzi wa Mama Dangote, Uncle Shamte amesema maswali ambayo wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu uhusiano wa mwanawe wa kambo Diamond Platnumz na malkia wa muziki Zuhura Othman almaarufu kama Zuchu yatajibiwa ifikapo Februari 14.
Akiwa kwenye mahojiano na Mbengo TV, Shamte alisema kwamba siku ya Valentines haitakuwa siku ya kawaida tu kwa Zuchu.
Shamte alifichua kwamba kuna jambo kubwa litakaloendekea siku ile na itafahamika kama ni kweli Diamond anakusudia kufungua ndoa na Zuchu.
"Swali kama tulipeleka barua ya uchumba litajibiwa tarehe 14. Mimi sio muongo, kuna tukio kubwa linaenda kutokea tarehe 14 ambalo linamhusu Zuchu" Uncle Shamte alisema.
Hivi majuzi uvumi uliibuka kuwa baba huyo wa kambo wa Diamond aliandamana na meneja Ricardo Momo pamoja na wazee kadhaa kutoka upande wa Diamond kupeleka barua ya uchumba nyumbani kwa kina Zuchu kama mojawapo ya maandalizi ya harusi kati ya wasanii hao wawili.
Shamte pia alisema anatamani sana kumwona Diamond akifunga pingu za maisha Nahuku akieleza kuwa atakuwa na furaha kubwa siku ambayo atapiga hatua hiyo.
"Furaha itapitiliza. Furaha huwa haijifichi, mtaiona. Mimi binafsi natamani nishuhudie kwa sababu namjua mwanangu. Napenda nimuone akifanya jambo hilo" Shamte alisema.
Shamte amekuwa kwenye mahusiano na mama ya Diamond, Bi Sanura Kassim almaarufu kama Mama Dangote kwa kipindi cha miaka kadhaa.