logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Siwezi jiumiza kwa ajili ya kiki,'Cartoon Comedian azungumza baada ya madai anatafuta kiki

kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikanusha madai kwamba anatafuta kiki.

image
na Radio Jambo

Habari09 February 2022 - 09:06

Muhtasari


  • Cartoon Comedian azungumza baada ya madai anatafuta kiki

Siku chache zilizopita mcheshi na muunda muadhui, Cartoon Comedian amekuwa akivuma mitandaoni baada ya kudai kuchapwa na baadhi ya watu ambao walikuwa wametumwa na mwanamuziki mmoja nchini.

Ni kawaida kwa wasanii,wacheshi kutafuta kiki wakati huu wa sasa ili vibao vyao vivume, madai yake mchesh huyo hayakuchukuliwa kwa uzito mwingi kwani asilimia kubwa ya wanamitandao waliai kwamba anatafuta kiki.

Cartoon alipakia video na picha akiwa amefura upande mmoja, na kusisitiza kwamba wasanii wanapaswa kutatua mambo yao na wala sio kutumana akapigwe.

Siku ya Jumanne kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikanusha madai kwamba anatafuta kiki.

PIa aliweka wazi kwamba hawezi jiumiza kwa ajili ya kiki, na kuwashukuru mashabiki wake kwa kuwa naye.

"Kwa nini nitafute kiki ilhali nina mashabiki wangu ambao wananishika mkono, kwa hivyo naweza jiumiza kwa ajoli ya kiki?tegeni maskio yenu," Aliandika Mcheshi huyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved