'Siwezi kuwa mpweke siku hii ya wapendanao,'Mwanamume atangaza kumpenda Betty Kyallo

Muhtasari
  • Betty yallo amjibu mwanamume aliyetangaza kumpenda
Betty Kyallo
Image: Instagram/Betty Kyallo

Mwanamume Mkenya aliyetambulika kwa jina la Skytone Baby anatafuta uchumba na Betty Kyallo,Skytone anasema ameamua kukiri haya  kwani Betty ndiye mwanamke anayefanya mapigo yake ya moyo kuongezeka.

Akiingia mitaani, Skytone aliandika bango akisema hataki kusherehekea siku ya wapendanao peke yake.

“Mimi ni Skytone baby, siwezi kuwa mpweke siku ya Valentine,Ninamtafuta mpenzi wangu, mrembo Betty Kyallo. Wana Nairobi wananiunganisha,” aliandika Skytone kabla ya kusambaza nambari yake.

Betty alijibu akisema atamtafuta Skytone baadaye ili wakanywe kahawa.

"Heri ya wapendanao wote. Pia kwa Muungwana huyu, asante kwa upendo. Acha nikununulie kahawa wakati mwingine."