Sijawahi tia unajisi nchini kenya-Rose Muhando

Muhtasari
  • Msanii wa njili Rose Muhando,amejitokeza wazi na kukataa madai kwamba amelala na mwanablogu Abraham Mutai

Msanii wa njili Rose Muhando,amejitokeza wazi na kukataa madai kwamba amelala na mwanablogu Abraham Mutai.

Kupitia simu iliyofanywa na kituo kimoja cha  redio nchini , mwimbaji maarufu alikataa kuwa na wakati mzuri na mfanyakazi wa mtandaoni katika moja ya makaazi.

Kwa mujibu wa Rose Muhando, hajawahi kukutana na mwanablogu huyo na hamjui.

Alikuwa kimya wakati uvumi ulipoanza  lakini alichagua kukaa kimya kwa sababu yeye hajibu  madai ya kijinga, aliongeza kwa kusema, kwamba mtu ambaye alieneza uvumi huo labada anamtamani.

"Mimi sijali na sijutii sababu sina hatia na wala sijawai kutia unajisi katika ardhi ya Kenya. Ajipange upya sababu amefeli

Huwa sijibu madai ya uongo kwa maana ni ya kijinga,simfahamu Abraham Mutai, na waa sijawahi lala naye Aseme tu kama ananipenda hapo sawa 

Kam walioniona kwenye vyumba vya kulala sina shida, kwa maana nikija Kenya lazima niende kwa vyumba vya kulala sina nyumba Kenya na kama wana ushahidi walete," Rose Muhando alijibu.