Familia ya Mwanamuziki na mwanasiasa mashuhuri kutoka Tanzania Joseph Haule almaarufu Profesa Jay imekanusha madai kuwa msanii huyo amefariki.
Kaka yake Profesa Jay, Black Rhyno akihojiwa na kituo kimoja cha habari, aliwambia mashabiki wa Profesa Jay wapuuza mbali madai yanayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na kuwa Profesa anaendelea kupata nafuu.
"Ni uongo. Hajafa. Tuache kusema mambo ambayo si ya kweli,"alisema Kakake Profesa.
Vilevile mwanasiasa wa Tanzania John Heche alizamia swala hilo ambapo alikana madai hayo akieleza kuwa bado Profesa Jay afya yake inaendelea kuimarika na hivyo watu wakome kueneza uvumi mbaya.
“Tunakuombea kupona tu ProfessorJayTz hatuna agenda nyingine nawe mtu wa watu Hatusikilizi maombi machafu ya wafuasi wa shetani, Damu ya yesu inanena mema kwako upone haraka,” alisema John Heche.