Karen Nyamu adokeza jinsia na jina la mtoto anayetarajia kujifungua

Muhtasari

•Nyamu amedokeza kuhusu jinsia ya mtoto ambaye anatarajia kujifungua hivi karibuni na jina ambalo atakusudia kumpatia.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Wakili na mwasiasa mashuhuri amedokeza kuhusu jinsia ya mtoto ambaye anatarajia kujifungua hivi karibuni na jina ambalo atakusudia kumpatia.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Nyamu amepakia video ya ujauzito wake na kuambatisha na ujumbe unaodokeza kuwa anatarajia mtoto wa kike.

Mama huyo wa watoto wawili ameendelea kudokeza kuwa jina la kitamaduni la mtoto wake litakuwa Njeri.

"Njeri anakuja.. nina raha sana" Nyamu aliandika.

Hata kama Nyamu hajafichua mengi kuhusu mtoto wake, wengi wameuchukua ujumbe wake kama dokezo la mtoto ambaye anatarajia.

Haya yanajri siku chache tu baada ya mgombeaji huyo wa kiti cha useneta wa Nairobi kwa tikiti ya UDA kuzua mdahalo mkubwa kuhusu ujauzito wake.

Karen alichapisha ujumbe ambao uliacha wanamitandao katika hali ya shaka kuhusiana na baba mzazi wa mtoto ambaye amebeba.

“Aache kujishuku, hajaambiwa mimba ni yake” Nyamu alijibu shabiki aliyezua madai kuwa nyota wa Mugithi Samidoh, ambaye anaaminika kuwa baba mzazi wa mtoto huyo alikana ujauzito.

Ujumbe wa Nyamu uliashiria kuwa huenda Samidoh hakuhusika kwenye ujauzito wa tatu wa Nyamu kama inavyotuhumiwa.