Penzi kikohozi ukificha chozi lasaliti , Zari ashindwa kulificha Gk Choppa ndiye dereva

Muhtasari

•Zari The Boss Lady ameamua kuweka penzi lake wazi baada ya kulificha kwa wiki kadhaa.

•Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz ameamua kumwaga yaliyomoyoni na kuonyesha  hadharani mpenzi wake mpya kwenye mtandao wa kijamii

Zari na Gk Choppa
Zari na Gk Choppa
Image: instagram/gk choppa

Mfanyabiashara na Mwanasosholaiti  mashuhuri Zari Hassani almaarufu Zari The Boss Lady ameamua kuweka penzi lake wazi baada ya kulificha kwa wiki kadhaa.

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz ameamua kumwaga yaliyomoyoni na kuonyesha  hadharani mpenzi wake mpya kwenye mtandao wa kijamii.

Pamoja na kukanusha mara si moja kuwa hawana mahusiano na mwanamume huyo, kweli tetesi hizo ziikuwa za kweli .

Si mwajua mapenzi kikohozi hayafichiki, Zari ameamua  kuweka uhusiano wake wazi na  Choppa.

Mama huyo wa watoto watano ameibui gumzo mtaani kwa kile wanamitandao wanasema anatoka kimapenzi na mwanamume aliyemzidi umri huku wengine  wakitabiri kuwa wataachana. 

Kupitia ukurusa wa instagram wa Gk Choppa, amepakia picha wakiwa pamoja na Zari huku wakipigana busu,  kitu ambacho kimewavutia wadaku wa mitandao.

Zari amefikia hatua ya kuonyesha mpenzi wake kwenye mtandao baada ya tetesi kuibuka kwamba Diamond anarusha roho na msanii  Zuchu.