'Usivuke mipaka,'Rayvanny amuonya Juma Lokole baada ya kumshambulia Fayvanny

Muhtasari
  • Mwimbaji kutoka Tanzania, Rayvanny amelazimika kumtetea mama wa mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii
Rayvanny
Image: HISANI

Mwimbaji kutoka Tanzania, Rayvanny amelazimika kumtetea mama wa mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii.

Hii ni baada ya mwanablogu maarufu Juma Lokole kumvamia kwenye mitandao yake ya kijamii.

Rayvanny alimtetea Fayvanny kwa kusema kwamba bado anamheshimu kwa hivyo Lokole hana haki ya kumvunjia heshima hadharani.

Rayvanny amekuwa akitamba kwa muda sasa.,Hii ni tangu alipoachana na Fayvanny na kuanza kumchumbia Paula Kajala.

Kwenye majukwaa yake ya mitandao ya kijamii, Rayvanny alishiriki machapisho kadhaa yanayoonyesha jinsi hakufurahishwa baada ya kutazama video iliyotumwa na Lokole kuhusu Fayvanny.

Kwenye posti hizo, Rayvanny alimwambia Lokole amheshimu mama wa mtoto wake.

Rayvanny aliendelea na kumsihi Juma kwamba amheshimu hivyo ajiepushe na kumshambulia Fayvanny.

"Juma Lokole tafadhali heshimu mama wa mtoto wangu, Sipendi,usivuke mipaka nakuheshimu sana," Aliandika Rayvanny.

Rayvanny hata hivyo aliendelea na kumwambia Juma kwamba hataki kupigana naye licha ya kile alichochapisha kuhusu Fayvanny.

"Nawaheshimu wote wawili,sipendi maneno,hii sio vita wala sio mambo ya mechi za mpira sipendi, na sipendi kabisa."