Mwanavlogu na mfanyibiashara Peter Kabi wa 'The Wajesus Family' alishirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu (Q&A) kwenye mtandao wa Instagram.
Maswali mengi yaliyoibuka katika kipindi hicho ni kuhusu ujauzito wa pili ambao mke wake Milly Wajesis amebeba kwa sasa.
Kabi alifichua kuwa mkewe anatarajiwa kubeba ujauzito huo kwa takriban mwezi mmoja unusu zaidi.
"Katika muda wa mwezi na wiki chache," Kabi alijibu shabiki aliyeuliza kuhusu wakati wanatarajia mtoto wao wa pili kuzaliwa.
Baba huyo wa watoto wawili wanaojulikana aliweka wazi kwamba bado hawajatambua jinsia ya mtoto ambaye wanatarajia.
"Bado hatujajua, tutafichua jinsia hivi karibuni," Kabi alijibu shabiki aliyekuwa na hamu ya kujua jinsia ya mtoto wao wa pili.
Kutokana na kura ambayo ilifanyika kwenye mtandao wa Instagram, Mashabiki wengi wa wanandoa hao wameonyesha kuwa wangependa wajaliwe mtoto wa kike.
Kabi amesema kuwa wazazi wao walipokea habari za ujauzio wa Milly kwa bashasha isiyo na kifani.
Pia ameweka wazi kuwa ujauzito huo wa mkewe haujamkazia kwa namna yoyote kufurahia haki zake za ndoa.
"Mimi bado nafurahia my conjugal right," Kabi alijibu shabiki aliyetaka kufahamu iwapo mtu anaweza kushiriki kitendo cha ndoa akiwa na ujauzito wa miezi saba.
Kabi na Milly walitangaza kuhusu ujauzito wa mtoto wao wa pili kwa njia ya kipekee mnamo mwezi Januari .