logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilikuwa nimekodisha nyumba ya ksh100 -Sandra Dacha asimulia kale yake

Sandra alieleza kuwa alikuwa anaishi kwenye vitongoji duni Korogocho

image
na

Makala04 March 2022 - 08:41

Muhtasari


•Mwigizaji na mpenzi wa Akuku Danger, Sandra Dacha amesimulia maisha aliyokumbana nayo wakati alipokuwa akiibukia kwenye tasnia ya uigizaji.

Sandra Dacha

Mwigizaji na mpenzi wa Akuku Danger, Sandra Dacha amesimulia maisha aliyokumbana nayo wakati alipokuwa akiibukia kwenye tasnia ya uigizaji.

Kupitia ukurusa wake wa instagram, Sandra alieleza kwamba alikuwa anaishi kwenye vitongoji duni Korogocho  ambapo alikuwa analipa kodi ya nyumba shillingi 100.

Mwigizaji huyo wa Auntie Boss mwenye ubunifu na ustadi  wa hali ya juu kuigiza alisema alielewa maisha ni hatua na yote hayo haliyapitia yanabaki kama kumbukizi kwake na mafunzo kwa wengine

Akisimulia a maisha yake alisema mapambano yake na maendeleo ya polepole yalifanya kuwa na imani kuwa kila kitu kinawezekana. 

 “Mwaka wa 2010 katika vitongoji duni vya Korogocho, hapa nilikuwa nimepanda daraja kutoka nyumba ya matope ambayo nilikuwa nalipa shilingi 100 tu, nilingia nyumba ya simiti ambayo nilikuwa nalipa shilingi 500, Nilikuwa nafurahia sana,”Sandra aliandika. 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved