Msako waanzishwa dhidi ya aliyerekodi Prof Jay akiwa ICU

Muhtasari

• Hospitali ya Kitaifa ya Muhimbili nchini Tanzania imesema imeshirikiana na mamlaka zingine ili kuanzisha msako wa kumpata aliyerekodi video ya Professor Jay akiwa hali mahututi kwenye sadaruki.

Professor Jay
Image: Malisa GJ (Facebook)

Baada ya manen makali kusambazwa mitandaoni kuhusu mkanda wqa video wqa msanii wa bongo fleva Professor Jay akiwa amelazwa katika kitanda cha ICU, sasa hospitali ya kitaifa nchini Tanzania ya Muhimbili ambayo awali ilikana kujua mwenye alirekodi video ile imesema kwamba imeanza uchunguzi wa kushirikiana na mamlaka nyingine ili kumjua mwenye alifanya mambo kama hayo ambayo yametajwa kuwa ukiukaji mkubwa wa kisheria na kimaadili.

Video hiyo iliyosambazwa mitandaoni inamuonesha msanii huyo akiwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum.

Hospitali hiyo imesema kwamba video husika haikurekodiwa na kusambazwa na hospitali, na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na imani nayo pamoja na kuheshimu taratibu za hospitali.

Awali, mwanaharakati wa haki za kibinadamu Malisa GJ aliibua madai mengi kupitia ukurasa wake wa Facebook akidai kwamba asilimia kubwa ya lawana zinatupiwa hospitali ya Muhimbili kwa sababu ni moja kati ya makundi matatu yaliyokuwa yameruhusiwa kuonana moja kwa moja na Jay, wengine wakiwa ni familia na maafisa kutoka serikalini.

Alisema kwamba vikundi hivyo vingine viwili si rahisi mtu arekodi video na hivyo kusema kama kuna mtuhumiwa mkubwa wa kurekodi video ile basi ni mmoja kati ya wahudumu wa hospitali ile wakiwemo madaktari na wauguzi.

Muhimbili baadae ilitoa taarifa ya kukana kuhusika katika kurekodi video hiyo na sasa imesema itashirikiana na mamlaka nyingine mpaka kuhakikisha mtu aliyeirekodi na kuisambaza video ile ametia nguvuni.