Muna Love adaiwa Tsh 8M za upasuaji wa kuongeza makalio

Muhtasari

• Baada ya kusema upasuaji wa kuongeza makalio nchini Uturuki ulimwendea mrama, mwanamama Muna Love sasa anasemekana kuwa na deni la milioni 8 kwa ajili ya sajari hiyo.

Muigizaji Muna Love
Muigizaji Muna Love
Image: Instagram

Madai mapya yameibuka kwamba Muna Love, mwanamama aliyeweka wazi kwamba alipata madhara makali kutokana na kufanya upasuaji wa kuongeza makalio sasa anadaiwa madeni ya upasuaji huo nchini Uturuki.

Muna Love inasemekana anadaiwa kiasi cha milioni nane za Kitanzania ambazo ni sehemu ya ada ya upasuaji huo uliomuendea mrama.

Pia inasemekana mwanamke huyo alipokwenda Uturuki kwa ajili ya upasuaji, aliangukia danga la kizungu ambaye wamekuwa wakiburudika na yeye.

Wiki chache zilizopita Muna aliweka wazi kwamba ada ya kufanya upasuaji huo ni ghali mno na kusema kwamba baada ya shughuli nzima kumuendea mrama, bado anazidi kujiuguza na pindi akipona ataelezea ukweli wa madhara ya ‘sajari’ hiyo.

Pia aliwausia vikali kina dad wanaofikiria kufanya upasuaji wa kuongeza viungo vya mwili na kubadilisha maumbile na kusema kwamba ni hatari kwa afya yao kwani ina madhara mengi tena mabaya kwa miili yao.