Rapa Noti Flow amkabidhi mpenziwe gari kama zawadi ya birthday

Muhtasari

ā€¢Notiflow amesema kuwa mapenzi yake kwa King Alami ni makubwa kuliko shilingi milioni 1.5 ambazo alitumia kumnunulia gari.

Image: INSTAGRAM// NOTI FLOW

Mwanamuziki Natalie Florence almaarufu Noti Flow amemnunulia mpenzi wake Armaan Alami (King Alami) gari kama zawadi ya siku ya kuzaliwa.

Rapa huyo alimzawadi mpenziwe gari aina ya Volkswagen anaposubiri kusherehekea siku yake ya kuzaliwa baadae wiki hii.

Akitangaza kuhusu zawadi hiyo, Notiflow amesema kuwa mapenzi yake kwa King Alami ni makubwa kuliko shilingi milioni 1.5 ambazo alitumia kumnunulia gari.

"Nilimsurprise mpenzi wangu kwa gari mpya kabisa aina ya Volkswagen UpšŸ¤© Siku yake ya kuzaliwa ni tarehe 25 lakini sikuweza kusubiri. King Alami nakupenda sana jamani. 1.5M si chochote ikilinganishwa na mapenzi niliyo nayo kwako. Ningekupa utajiri wangu wote kama singekuwa na majukumu," Noti Flow alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Noti Flow na King Alami ambao ni wapenzi wa jinsia moja wamekuwa kwenye mahusiano kwa takriban mwaka mmoja. Rapa huyo alijitambulisha kama msagaji mnamo mwezi Mei mwaka jana .

Mwaka jana, wawili hao walikuwa wametengana kwa muda ila baadae wakarudiana na kuendeleza mahusiano yao.