Esma Platnumz azungumzia madai ya Aaliyah kuwa na ujauzito wa Diamond

Muhtasari

•Alisema hana ufahamu wowote kuhusu mahusiano yoyote ya  kimapenzi kati ya kakake Diamond Platnumz na mtangazaji Aaliyah Mohamed.

•Aliweka wazi kuwa huwa anamuona Aaliyah mara kwa mara ila bado hajaona dalili zozote za ujauzito kwake.

Diamond Platnumz na Aaliyah Mohamed
Diamond Platnumz na Aaliyah Mohamed
Image: HISANI

Mfanyibiashara Esma Platnumz amesema hana ufahamu wowote kuhusu mahusiano yoyote ya  kimapenzi kati ya kakake Diamond Platnumz na mtangazaji Aaliyah Mohamed.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuzindua video za EP ya FOA, Esma alisema hana uhakika kuhusu jinsi wawili hao wanavyohusiana licha wa karibu nao.

"Aaliyah ni jirani wangu kabisa. Huwa tunaonana na saa zingine huwa tunalala pamoja. Mimi kuwa na Aaliyah sio tatizo. Habari za mimba mimi sijui, na sijui kama ana mahusiano na Naseeb, sijui chochote," Esma alisema.

Mama huyo wa watoto wawili aliweka wazi kuwa huwa anamuona Aaliyah mara kwa mara ila bado hajaona dalili zozote za ujauzito kwake. 

"Aaliyah hana mimba. Namuona yuko kawaida. Yeye ni rafiki yangu, tunakaa katika nyumba moja. Sisi ni majirani na sijaona mimba, sijaona kukata breed," Alisema.

Tetesi kwamba mtangazaji huyo ana mahusiano ya kimapenzi na bosi wake katika Wasafi Media, Diamond zimekuwa zikienezwa kwa muda mrefu.

Mwaka jana madai yaliibuka kwamba wawili hao wanatarajia mtoto pamoja.