Baba Levo: Daimondi akifa nitalia kuliko Zuchu

Muhtasari

Daimondi akifa nitalia kuliko Zuchu..!! maana tangu ameanza kunisaidia maisha yangu na watoto wangu yamebadilika kabisa..!! maana tangu ameanza kunisaidia maisha yangu na watoto wangu yamebadilika kabisa

Baba Levo na wasanii Diamond na Zuchu
Baba Levo na wasanii Diamond na Zuchu
Image: INSTAGRAM

Msanii mwenye utata mwingi kutokea bongo Tanzania, Baba Levo amezua mapya kabisa ambayo yamelichemsha gumzo zito kuhusu uwezekano wa Diamond Platnumz kuwa katika mahusiano na Zuchu.

Baba Levo ameandika ujumbe wenye ukakasi kwenye Instagram yake akisema kwamba Diamond akifa atabubujikwa zaidi na machozi kuliko msanii Zuchu ambaye kwa siku za hivi karibuni ameonekana kuwa na ukaribu usio wa kawaida na bosi wake Diamond Platnumz.

Baba Levo aidha hajaweka wazi kama anamtakia Diamond kifo au vipi lakini amefafanua kwa kiduchu tu kwamba kulia kwake kwa wingi mpaka kushinda taji na muombolezaji ‘bora’ zaidi ya mtu yeyote yule ni kwa sababu ya heshima zake kwa Simba ambaye alimsaidia na kumuaminia wakati hakuna mtu alitaka kufanya kazi na yeye.

“Daimondi akifa nitalia kuliko Zuchu..!! maana tangu ameanza kunisaidia maisha yangu na watoto wangu yamebadilika kabisa. thanks @diamondplatnumz mungu akuongezee ..! tunakuombea sana..!” Aliandika Baba Levo kwenye Instagram yake.

Wengi wameonekana kutoelewa pointi ya Baba Levo hapa huku baadhi wakidai kwani ukiwa unamheshimu mtu mpaka umtakie kifo ili uje kudhihirisha heshima hizo wakati wa msiba wake.

Sijui wewe unalitafakari vipi hili!