Dadake Diamond, Esma Platnumz azungumzia suala la mahusiano yake na Zuchu

Muhtasari

•Mama huyo wa wawili  aliidhinisha mahusiano kati ya mastaa hao wawili wa Bongo huku akisema wanafaana.

Diamond na Zuchu
Diamond na Zuchu
Image: KWA HISANI

Mfanyibiashara Esma Abdul almaarufu Esma Platnumz ameapa kwamba kamwe hawezi kuingilia mahusiano ya kakake Diamond Platnumz.

Hivi majuzi akihutubia waandishi wa habari katika ukumbi wa Mlimani City, Esma aliweka wazi kwamba hana uhakika wowote  kuhusu mahusiano ya kimapenzi yanayodaiwa kati ya kakake na Zuchu.

"Sina uhakika kwamba ni wapenzi. Ninachokijua mimi ni kuwa ni mtu na bosi wake," Esma alisema.

Mama huyo wa wawili hata hivyo  aliidhinisha mahusiano kati ya mastaa hao wawili wa Bongo huku akisema wanafaana.

Esma aliweka wazi kuwa wawili hao, Diamond na Zuchu wapo single kwa sasa.

"Sio mbaya. Yule ni mwanamke na mwanaume. Mwanaume yuko Single na mwanamke yuko single, sio mbaya," Alisema.

Esma alieleza kuwa familia yake ikiwemo yeye na Mama Dangote inahusika tu katika kuunga mkono kazi za Diamond ila sio kuingilia mahusiano yake.