logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Betty Kyallo azungumzia suala la ushirikiano katika malezi na aliyekuwa mumewe Dennis Okari

Alisema kila mmoja wao huwa anapata muda wa kukaa na binti yao na huwa wanahudhuria mikutano yake pamoja.

image
na Radio Jambo

Makala28 March 2022 - 07:15

Muhtasari


•Betty amefichua kwamba kuna ushirikiano mzuri kati yake na Okari katika malezi ya binti yao wa miaka saba, Ivanna.

•Alifichua kwamba kila mmoja wao huwa anapata muda wa kukaa na binti yao na huwa wanahudhuria mikutano yake shuleni pamoja.

Dennis Okari na aliyekuwa mkewe Betty Kyallo

Mtangazaji na mfanyibiashara mashuhuri Betty Kyallo ameweka wazi kwamba hakuna uhasama wowote kati yake na aliyekuwa mumewe Dennis Okari.

Betty amefichua kwamba kuna ushirikiano mzuri kati yake na Okari katika malezi ya binti yao wa miaka saba, Ivanna.

"Kushirikiana katika malezi kumekuwa kuzuri. Ivanna anampenda sana babake na babake vilevile anampenda," Betty alisema akiwa kwenye mahojiano na Citizen Digital.

Mtangazaji huyo ambaye alitimiza miaka 33 hivi majuzi hata hivyo amekiri kwamba ilichukua muda kabla yao kuweza kushirikiana vizuri baada ya ndoa yao kugonga ukuta takriban miaka mitano iliyopita.

Alifichua kwamba kila mmoja wao huwa anapata muda wa kukaa na binti yao na huwa wanahudhuria mikutano yake shuleni pamoja.

"Huwa tunaenda na Dennis kwenye mikutano yote ya shule. Jinsi huwa tunaketi watu wanaweza kufikiri bado tuko pamoja. Hatuna ugomvi. Sisi ni marafiki. Huwa tunapigiana simu kila wakati kuhusiana na binti yetu," Alisema.

Betty ameweka wazi kwamba kwa sasa yupo single na bado anamtafuta mwanaume atakayestahiki kuwa baba mzuri kwa binti yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved