EX wangu wote wanajua kusoma katiba vizuri-Huddah Monroe amwaya mtama

Muhtasari
  • Huddah aliweka wazi kwamba kile anachohitaji kutoka kwa mwanamume ni heshima na uaminifu
Image: INSTAGRAM// HUDDAH MONROE

Mwanasosholaiti maarufu nchini Huddah Monroe kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ameewasifia ex wake.

Kulingana na majasirimali huyo ex wake wote walikuwa wanajua kusoma katiba, huku akiwasuta marafiki wanawake ambao walikuwa wanawamezea wanaume wake mate.

Aidha alijisifu na kusema kwamba anajua kuchagua wanaume wazuri, ndio maana marafiki zake walikuwa wanawatamani.

Huddah aliweka wazi kwamba kile anachohitaji kutoka kwa mwanamume ni heshima na uaminifu na wala sio kitu kingine.

"Kitu pekee ninchohitaji kwa mwanamume ni uaminifu na heshima, wengi wamo humu nje lakini hawana ladha,marafiki zangu wa kitambo walikuwa wanawamezea mate na kuwatafuta ex wangu kwani walijua huwa nachagua vyema na wanaume wazi

Ex wangu wote wanajua kusoma katiba," Aliandika Huddah.

Huddah alitoa sababu kuu ya kutopakia mwanamume wake mitandaoni.

"Hii ndio sababu huwa sipakii mwanamume wangu mitandaoni, kwa maana wanawake watamtamani, lakini nitapakia mmoja hivi karibuni."