Je, Harmonize anamkosa Kajala? Vipi kuonekana kwenye bango?

Muhtasari

• "Unaweza niona na niamini mimi, sina furaha. Kila mtu katika Konde Gang anajua kwamba nakukosa sana" - Harmonize 

Harmonize
Harmonize
Image: Mudu Moh, Facebook

Baada ya uvumi kusambaa mitandaoni kwamba msanii Harmonize bado analikosa sana penzi na uwepo wa muigizaji mkongwe wa filamu za bongo, mwanamama Fridah Kajala, hatimaye msanii huyo amelitema dukuduku lake la moyoni.

Wikendi iliyopita, aliachia ujumbe tata kwenye instastories zake ambapo aliweka wazi kwamba anamkosa sana Kajala katika maisha yake licha ya kuwa katika penzi lingine na mwanadada mzungu.

“Unaweza niona na niamini mimi, sina furaha. Kila mtu katika Konde Gang anajua kwamba nakukosa sana,” aliandika harmonize.

Japo hakumtaja mlengwa wa ujumbe wenyewe, lakini wengi walihisi kwamba huu ujumbe kwa njia yoyote ile utakuwa umeelekezwa kwa Kajala.

Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kubainisha na kudhihirisha wazi mapenzi yake kwa mwanamama Kajala ambaye kwa wakati mmoja walikuwa katika mapenzi kabla ya Sakata la Harmonize kumtaka kimapenzi mwanawe Kajala, Paula ambaye ni mpenzi wa Rayvanny.

Tetesi hizi kuhusu kumkosa Kajala zinakuja muda mchache tu baada ya bango kubwa kuonekana Harmonize akiwa na Kajala ambapo limeambatanishwa na neno “Lovers”