Zuchu amrukia shabiki aliyedai hajui kuandika jina 'MUNGU'

Muhtasari

• Na ubaya huo unaoniona nao ninaishi kwenye hekalu nina gari mbili, ya tatu nimeagiza yaja. A superstar ndio maana uko hapa unacomment - Zuchu kwa shabiki aliyemchamba.

malkia wa bongo fleva, Zuchu
malkia wa bongo fleva, Zuchu
Image: INSTAGRAM

Unaambiwa ukiwa maarufu basi mashabiki wako lazima watakuwa wanakufuatilia kwa ukaribu sana tena kwa macho ya umakini kama mwewe katika kila jambo unalolifanya, haswa katika mitandao ya kijamii.

Wikendi iliyopita, msanii Zuchu alipakia kwenye Instagram yake kama kawaida na ambapo aliandika ‘caption’ ambayo shabiki mmoja aliiona kwamba hajaandika jina ‘Mungu’ vizuri.

Shabiki huyo ambaye alishindwa kukaa na hilo dukuduku moyoni aliamua liwe liwalo na kumpasha Zuchu kwa kumsuta kwamba licha ya ukali wote lakini ameshindwa kuandika neno Mungu vizuri eti.

“Neno Mungu limekushinda kuandika ila wewe ulikuwa mbaya hadi nakuzidi,” shabiki huyo kwa jina Shannyog4 aliandika.

Maoni haya ni kama hayakuenda vyema kwa upande wa msanii Zuchu ambaye aliamua kumpasha shabiki huyo na kumnyamazisha ghafla.

“Na ubaya huo unaoniona nao ninaishi kwenye hekalu nina gari mbili, ya tatu nimeagiza yaja. A superstar ndio maana uko hapa unacomment… nasubiri vyako udugu uliyenizidi uzuri,” aliandika Zuchu.

Kwani mtajuaje huyu ni mtoto wa malkia wa mipasho Khadija Kopa, kama hatawapasha mkiingia kwenye kumi na nane zake?