David Moya: Huddah ndio 'celebrity crush' wangu

Muhtasari

• Mcheza densi Moya David alisema mtu mashuhuri ambaye anamkodolea macho ya tamaa ni mwanasosholaiti Huddah Monroe na kusema kwamba anatamani kucheza densi na yeye waakti mmoja.

David Moya, Huddah Monroe
David Moya, Huddah Monroe
Image: Instagram

Jamaa mcheshi anayejulikana sana kwa kushtukiza kwenye shughuli za watu na kuanza kusaka densi huku akiwakabidhi maua, David Moya anasema kwamba anamtamani sana mwanasosholaiti Huddah Monroe na kukiri kwamba siku moja atampigia simu kuomba nafasi ya kumchezea densi, na pengine kumkabidhi maua.

Moya ambaye alikuwa akifunguka haya katika kipindi cha mchekeshaji Oga Obinna kwenye mtandao wa YouTube, alisema kwamba amechezea densi watu wengi tena mashuhuri lakini bado mmoja tu na ambaye ni mjasiriamali vya vipodozi, Huddah.

“Nani celebrity crush wako, kwa sababu nilikuona na Corazon, Frankie hata hajatoka na wewe tayari umefika pale unamchezea densi na kumpa maua. Ni mtu yupi mashuhuri ambaye unasema ukimpata tu utaacha kucheza densi?” aliuliza Obinna.

“Wako wengi lakini mimi nadhani, Huddah. Tumekutana na yeye awali na kuchukua picha za pamoja lakini kwa sasa nataka tu kucheza densi na yeye,” alijibu Moya baada ya kuguna kwa muda.

Kijana huyo aligonga vichwa vya habari za burudani kote nchini baada ya kuwa mcheza densi wa kujitegemea wa kwanza kuwahi kufikisha wafuasi zaidi ya milioni moja kwenye mtandao wa TikTok wiki chache zilizopita.