"Unavaa ka mumama kwani wee ni wa mashambani?" Sosuun amjibu Vivianne

Muhtasari

• I could have In-law problems fine but wewe zalia bwanako mtoto tuone vile utakua unafanya kwa hii industry ya Kenya ya double standards - Sosuun amjibu Vivianne.

Msanii wa kufoka Sosuun na msanii mwenza Vivianne
Msanii wa kufoka Sosuun na msanii mwenza Vivianne
Image: Instagram

Ugomvi ulioonekana kama mzaha baina ya wanamuziki Vivianne na Sosuun unaonekana kukolea zaidi ya kuwa wa kikweli baada ya wengi kudai kwamba wawili hao ni kiki walikuwa wanatafuta awali.

Vivianne ndiye aliyeanza chokoza zake kwa Sosuun kwa kuuliza ni kwa nini ametulia sana bila kusikika katika kufanya ngoma kwa muda sasa. Ikumbukwe Jumatatu ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Sosuun na Vivianne alimtakia kheri njema huku akimpa changamoto ya kuasi ukimya na kutoa kibao kipya.

“Nimesoma place ni birthday ya Sosuun. Happy birthday to her. I found out about this mama akiangusha mistari pale grandpa. Flow hatari but kwani mistari ziliisha? It is such a shame gift kama ya huyu dem ikidissapear nkt. Unachukua break 10 years, how will we remember you surely” alichokoza Vivianne.

Baada ya saa kadhaa, msanii Sosuun alijiweka tayari na kuliachia bomu kali kwa Vivianne.

“Industry yenyu hata mtu aawaachie bado tu mnamtafuta, now #Vivian Mimi na wewe tunaulizana Nini?  First, up your game ukae super star ndio tuongee Mimi na wewe, check your wardrobe you are still very young kuvaa ka mumama kwani wewe ni msanii wa mashambani? , I could have In-law problems fine but wewe zalia bwanako mtoto tuone vile utakua unafanya kwa hii industry ya Kenya ya double standards, you think it's easy coz you ain't in my shoes.  I can assure you huwezi nikosea heshima wewe, this I promise I'll get hold of you and it will be messy...!” alijibu mipigo Sosun.

Baadhi ya mashabiki wa muziki wa humu nchini bado wanaamini kwamba wawili hawa wanajaribu kuvutia umakini wa mashabiki kama mojawapo ya maandalizi ya kuachia ngoma mpya, ila wengine pia wanahisi huu ni ugomvi wa kweli ambao ulioteshwa moto na Vivianne.