Vera Sidika afichua uhusiano wake mrefu zaidi wa kimapenzi

Muhtasari
  • Vera Sidika afichua uhusiano wake mrefu zaidi wa kimapenzi
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti maarufu nchini Vera Sidika anafahamika kwa shepu ya mwili wake na urembo wake wa kipekee.

Vera amekuwa akigonga vichwa vya habari mitandaoni kila mara kwa jambo moja au lingine.

Mwanasosholaiti huyo amebarikiwa na mtoto wa kike ambaye anasifika kwa urembo wake.

Takriban miezi mitano tu baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza, mwanasoshalaiti Vera Sidika amedokeza kwamba huenda tukamuona amebeba ujauzito mwingine hivi karibuni.

Vera amefichua kwamba mahusiano yake na Mauzo ndiyo marefu zaidi kuwahi kuwa nayo katika maisha yote akiwa mtu mzima.

"Uhusiano wa kimapenzi mrefu zaidi ambao nimewahi kuwa nao, ni huu wangu moenzi wa maisha yangu, katika miezi nne ijayo tutakuwa tukisherehekea au kuadhimisha miaka 2 katika uhusiano

Nina tamaa kubwa ya mtoto. Kweli, sio mimi tu, mume wangi  pia. Tunataka mtoto mwingine. Kwa matumaini, mvulana. Labda tunapaswa kuzingatia hilo  na kujaribu. Kwa kiwango hiki, Mtu huenda akawa mjamzito tena mwaka huu,"Sidika Aliandika.