DeSagu adai Spaghetti ilipunguzwa idadi kutoka 210 hadi 191

Muhtasari

• Mchekeshaji Henry DeSagu alilalamika kwamba si tu mafujta ambayo yamepanda bei bali hata watengenezaji wa chakula aina ya Spaghetti walipunguza njiti hizo kutoka 210 hadi 191.

Mchekeshaji Henry DeSagu
Mchekeshaji Henry DeSagu
Image: Facebook

Mchekeshaji Henry DeSagu anateta kwamba maisha yanazidi kuwa magumu humu nchini si tu kwa uhaba wa petroli ambao madhara yake yanawakodolea Wakenya wengi macho katika kipindi hiki baki pia katika vyakula.

DeSagu akilalamika kupitia Facebook yake, ameteta kwamba kampuni ya kutengeneza Spaghetti pia ilifanya hujuma kwa wateja wake kwa kupunguza kiwango cha chakula hicho eti.

Kulingana na DeSagu, umakini wake ulimtuma kucvhukua hesabu ya Spaghetti ambazo aligundua kwamba kiwango chake kimepungua kutoka njiti 210 za Spaghetti na eti sasa baada ya kuhesabu alipata zimepungua mpaka njiti 191 kutoka idadi ya awali.

“Si kawi pekee, walipunguza idadi ya njiti za spaghetti kutoka 210 hadi 191,” aliandika DeSagu huku akifuatisha maneno hayo na emoji ya kulia.

Taifa la Kenya linaelekea katika hali mbaya ya kiuchumi baada ya uhaba wa petroli kubisha hodi katika maeneo mengi ambapo shughuli muhimu zimekwama, ikizingatiwa kwamba bidhaa ya petroli hutumika katika kuendesha shughuli viwandani na barabarani.

Haya yanakuja wiki kadhaa tu baada ya baadhi ya wakenya kuanzisha maandamano ya mitandaoni wakitaka bei ya vyakula kupunguzwa almaarufu #Lowerfoodprices.