Fahamu kwa nini mamake Diamond Platnumz anamsukuma afunge ndoa mwezi huu

Muhtasari

•Mama Dangote amemtaka mwanawe amvishe pete mpenzi wake baada ya mwezi mtukufu wa wa Ramadhan.

•Mama Dangote aliweka wazi kwamba amemkubali mpenzi wa Diamond na kumshauri atulie sasa na afunge pingu za maisha naye.

Diamond Platnumz na mamake Mama Dangote
Diamond Platnumz na mamake Mama Dangote
Image: HISANI

Bi Sanura Kassim almaarufu kama Mama Dangote ameendelea kumshinikiza mwanawe, Diamond Platnumz kufanya hara kufunga ndoa na mchumba wake.

Mama Dangote amemtaka mwanawe amvishe pete mpenzi wake baada ya mwezi mtukufu wa wa Ramadhan.

Kulingana na Mama Dangote, Kuna nafasi kubwa la Diamond kupokea baraka zisizo na mwisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika msimu huu wa sikukuu.

"Mara nyingine tena narudia Nasibu Diamond Platnumz, Mfunge ndoa mwezi huu ukiisha maana baraka zake Allah ndio anazijua," Mama Dangote alimwambia Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Haya yanajiri baada ya mke huyo wa sasa wa Uncle Shamte kueleza kuridhika kwake na mchumba mpya wa mwanawe ambaye hajatambulishwa.

Mama Dangote aliweka wazi kwamba amemkubali mpenzi mpya wa Diamond na kumshauri atulie sasa na afunge pingu za maisha naye.

"Nashindwa kuelezea furaha yangu mwanangu, Naseeb Diamond Platnumz🦁, hapa sasa umepata mwenza. Utulie babangu uoe," Mama Dangote alisema.

Haya yanajiri huku kukiwa na tetesi kwamba bosi huyo wa WCB alifunga pingu za maisha na mwanadada kutoka Zanzibar katika harusi ya siri.