logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Huyu sasa ndiye wa maisha!" Babake Diamond amkubali mpenzi wake mpya

Uncle Shamte ameeleza kuridhishwa kwake na mpenzi mpya wa staa huyo wa Bongo.

image
na Samuel Maina

Burudani05 April 2022 - 04:41

Muhtasari


  • •Amemtakia mwanawe mema katika ndoa yake na kutangaza wazi kuwa angependa mpenzi huyo mpya wa Diamond  awe mkewe wa maisha.

Baba wa kambo wa Diamond Platnumz, Uncle Shamte ameeleza kuridhishwa kwake na mpenzi mpya wa staa huyo wa Bongo.

Uncle Shamte ambaye ni mume wa sasa wa Mama Dangote ameweka wazi kwamba amempokea malkia huyo ambaye hajatambulishwa kwa mikono miwili.

Amemtakia mwanawe mema katika ndoa yake na kutangaza wazi kuwa angependa mpenzi huyo mpya wa Diamond  awe mkewe wa maisha.

"Siwezi kusema atakuwa Mke wa Uji ila Leo umenidhihirishia ukubwa wako Simba, akawe wa milele🙌 huyu sasa ndio wa Maisha nimempokea kwa mikono miwili🤲 Kwa alivyonyooka hivi atakuwa wa wapi huyu?" Shamte alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Shamte anaunga mkono kauli ya mkewe, Mama Dangote ambaye alimshauri Diamond afunge pingu za maisha na kipenzi hicho chake kipya.

Mama Dangote alieleza kuridhishwa kwake na mwanadada huyo asiyetambulishwa na kumpokea katika familia yake kwa mikono miwili.

"Nashindwa kuelezea furaha yangu mwanangu, Naseeb Diamond Platnumz🦁, hapa sasa umepata mwenza. Utulie babangu uoe," Mama Dangote alisema.

Jumbe za wanandoa hao wawili zimeibua tetesi kwamba huenda Diamond alifunga ndoa kisiri. Wengi wanasubiri kwa hamu kumtambua malkia mpya kwenye ufalme wa Simba.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved