"Mjinga sana!" Juma Lokole amlipukia Harmonize kwa kumpa Diamond tuzo

Muhtasari

• Mtangazaji mwenye umbea Juma Lokole amemlipukia msanii Harmonize kwa kitendo chake cha kumpa Diamond tuzo moja  kisa alishinda tatu naye Mond akapewa moja.

Harmonize, Juma Lokole
Harmonize, Juma Lokole
Image: Instagram

Mtangazaji mwenye udaku na umbeya uliopitiliza Juma Lokole ameamua kuupalilia ugomvi wa maneno kati ya bosi wake Diamond Platnumz na mkurugnzi mtendaji wa rekodi lebo ya Konde Gang, Harmonize.

Jumatatu Juma Lokole amemlipua vikali kwa baruti msanii Harmonize kwa kile alisema kwamba kitendo na Harmonize kuikabidhi moja ya tuzo yake kwa msanii Diamond si mapenzi ya dhati kama alivyodokeza bali ni kujipendekesha na kujionesha tu kwamba ana fadhila lakini hamna kitu.

Japo alizungumza bila kulitaja jina la Harmonize, kila mtu aliyefuatilia kwa ukaribu matukio wikendi iliyopita katika hafla ya tuzo za TMA aliju fika kwamba maneno yake yalikuwa yanamlenga moja kwa moja Harmonize.

“Kuna watu walipanda stejini pale wakamdhihaki Diamond ati ooh mimi nimeshinda tuzo tatu sio picha nzuri halafu Diamond kupewa tuzo moja kwa hiyo acha hii moja nimpe… tunajua kiunafiki tu lakini tumwambie ukweli, shule muhimu. Tuzo aliyopewa Diamond ni kubwa kuliko hata hizo tatu ulipewa za mchongo,” Juma alimkashfu Harmonize.

Juma alizidi kufafanua kwamba tuzo aliyokabidhiwa Diamond ni ya heshima kwa kuutangaza muziki wa bongo kimataifa na ni zaidi ya tuzo zozote zilizotolewa kwa wasanii wa kawaida.

Aliwataja baadhi ya watu wachache tu ambao waliwahi pokezwa tuzo za heshima kama ile na kusema kwamba Diamond ameingia kwenye kurasa za marehemu Rais Samia Suluhu, Ruge Mtahaba, Bi Kidude miongoni mwa wengine wachache ambao waliwahi kutambulika kwa tuzo za heshima.