Mwanaume afungwa miaka 24 jela kwa kukiri kutotambua uwepo wa Mungu

Muhtasari

• Mubarak Bala, Mnigeria aliyekana uwepo wa Mungu alikabidhiwa kibano cha miaka 24 jela kwa kuenda kinyume na sheria za dini ya Kiislam.

• Mashirika ya kutetea haki za Kibinadamu yamekshfu kifungo hicho na kutaka aachilie mara moja.

Picha ya Mubarak Bala, kafiri aliyetangaza kutotambua Mungu
Picha ya Mubarak Bala, kafiri aliyetangaza kutotambua Mungu
Image: BBC NEWS//AFP

Jamaa mmoja muislam nchini Nigeria amejipata katika upande mbaya wa sheria za nchi hiyo baada ya kukana kutambua uwepo wa Mungu na hivyo kupigwa kibano cha miaka 24 jela.

Mubarak Bala mwenye umri wa miaka 37 anasemekana kukana hadharani kutotambua uwepo wa Mungu mnamo mwaka 2014 na mwaka wa 2020 alitiwa nguvuni ambapo alishtakiwa kwa makosa 18 yanayohusiana na kukiuka taratibu za dini ya Kiislam na kumkana Mungu, mashtaka ambayo aliyakubali yote bila kutetereka ila akaomba mahakama impe msamaha.

Bala alijipata katika mchezo wa paka na panya na sheria baada ya watu wa jamii ya Kiislam kutoka taifa la Nigeria kuwasilisha ombi la kutaka akamatwe kwa kile walisema ni kupakia jumbe zilizokuwa zikilichafua jina la dini ya Kiislam.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la BBC, Bala ni mkaazi wa eneo la Kano ambalo liko kaskazini mwa taifa la Nigeria ambapo idadi kubwa ya wakaazi ni Waislam.

Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu kutoka UN na makundi mengine ya kimataifa ya haki za binadamu yamelaani kifungo hicho huku wakitaka Bala aachiliwe huru, ambapo madai mengine yanasema kafiri huyo angehukumiwa kifo kama angeshtakiwa katika mahakama ya Kiislamu.

Taifa la Nigeria ni moja kati ya mataifa ya Afrika yenye idadi kubwa ya watu ambapo limegawanyika mara mbili kidini, sehemu ya Kaskazini ambayo iko katika misukosuko ya vita na mshambulizi ya wanamgambo wa Boko haram ikiwa na idadi kubwa ya Waislam huku sehemu ya Kusini yenye utajiri mkubwa wa mafuta ikitawaliwa na idadi kubwa ya Waislamu.