(Screenshot) Anerlisa aeleza jinsi mpenzi wake anamdekeza kwa mapenzi

Muhtasari

• Anerlisa Muigai aliachana na msanii Ben Pol siku chache baada ya kufanya harusi ya Kikatoliki.

• Kando na kuwa mrithi wa Keroche, ana kampuni yake binafsi inayojihushisha na masuala ya kupakia maji kwa jina la Nero.

Mrithi wa Keroche, Anerlisa Muigai
Mrithi wa Keroche, Anerlisa Muigai
Image: Instagram

Baada ya kuachana na mwanamuziki kutoka Tanzania, Ben Pol, mrithi wa kampuni ya kutengenezxa vileo Keroche Breweries, Anerlisa Muigai hatimaye amepata wa kumpa shavu la mapenzi na amani ya moyo na nafsi.

Mwanamke huyo ambaye kuachana kwake na Ben Pol kulijiri siku chache tu baada ya ndoa takatifu kulimsababishia msanii huyo kuvunjika moyo vibaya sana mpaka kubadilisha dini kutoka ya Kikristu kuelekea ile ya Kiislamu.

Anerlisa ambaye pia kando na kuwa mrithi wa Keroche, ana kampuni yake binafsi inayojihushisha na masuala ya kupakia maji kwa jina la Nero.

Katika siku za hivi karibuni, Anerlisa amekuwa akiwatania wanamitandao kuhusu mpenzi wake mya ambaye alidinda sana kutambulisha uso wake kwa ‘mashemeji’ wa mitandaoni. Alikuwa anapakia picha za pamoja huku akiwa amemficha uso kweli kweli kama siri lakini wakati mmoja juzi kati hapa alionesha video ya mpenzi huyo wake wakati walikuwa katika hafla moja ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Rafiki yake.

Ijumaa Anerlisa amepakia ‘meme’ kwenye Instagram yake ikiwa na mkono unaolishikilia yai kwa mtindo wa kudekeza vile ambapo inafuatishwa na maneno kwamba inaashiria kwa uhalisia jinsi mpenzi wake mpya anavyomdekeza na kumhendo kwa mapenzi yasiyojua kufa.

“Picha muhali sana inayotoa maelezo jinsi mpenzi wangu anavyonidekeza na kunihendo,” maneno hayo yanasema.

Anerlisa ambaye kampuni yao ya vileo Keroche imekuwa na mfarakano mkali na mamlaka ya ukusanyaji kodi, KRA kutokana na malimbikizi ya madeni ya ushuru alidokeza kwamba uamuzi wake wa kuhamia jijini Nakuru ni kutokana na kwamba mji huo una amani sana na amani ndio kama kitu kipya ndani yake anachokienzi sana.

screenshot
screenshot