Hatimaye Carol Sonnie avunja kimya kufutia madai ya kushangaza ya Mulamwah dhidi yake

Muhtasari

•Muthoni amezamia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuchapisha ujumbe ambao umeoneka kuzungumzia yale yanayoendelea.

•Hapo awali Muthoni alipotembelea studio zetu alisisitiza kwamba yupo tayari kufanya DNA iwapo itabidi.

Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Carrol Sonnie katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Hatimaye mwigizaji Caroline Muthoni amezungumza baada ya aliyekuwa mpenzi wake David Oyando almaarufu Mulamwah kuibua kapu la madai ya kushangaza kumhusu.

Hivi majuzi Mulamwah alimshtumu Muthoni kwa kutokuwa mwaminifu wakati wa mahusiano yao, kupachikwa ujauzito na jamaa mwingine kati ya madai mengine mengi.

Muthoni amezamia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuchapisha ujumbe ambao umeoneka kuzungumzia yale yanayoendelea.

"Maisha yanapokupa sababu mia za kuangua kwa kilio, onyesha maisha kuwa una sababu milioni za kutabasamu na kushukuru. Kuwa na nguvu," Muthoni aliandika.

Mulamwah alishangaza wengi siku ya Ijumaa baada ya kudai kwamba yeye sio baba mzazi wa binti wa Muthoni. 

Wanamitandao wameendelea kutoa hisia tofauti kuhusiana na madai hayo, baadhi wakimshtumu huku wengine wakipendekeza vipimo vya DNA vifanyike.

Hapo awali Muthoni alipotembelea studio zetu alisisitiza kwamba yupo tayari kufanya DNA iwapo itabidi.

Kwa kipindi cha takriban miezi sita ambacho kimepita Mulamwah amekuwa akisisitiza kwamba  mtoto huyo ni wake hadi Ijumaa alipobadilisha msimamo.