logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Leo nitamtambulisha nimpendae,'Diamond awaambia mashabiki

"Panapo maajaliwa leo nitamtambulisha nimpendae,niliezama kwenye huba na kuridhia nae,

image
na Radio Jambo

Habari11 April 2022 - 10:50

Muhtasari


  • Diamond Platnumz aahidi kutambulisha mpenzii wake

Kwa muda sasa staa wa bongo Diamond Platnumz amekuwa akigonga vichwa vya habari, baada ya madai kwamba amempata ampendaye.

Huku uvumi wa ndoa yake ukienea na kuvuma sana, msanii huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewaambia mashabiki wake kwamba majaliwa siku ya Jumatatu atamtambulisha mpenzi wake.

Jumapili, Diamond alitangaza kwamba kitakachokuwa kinaendelea usiku huo kitapeperushwa moja kwa moja kwenye runinga yake Wasafi TV kwa minajili ya wale ambao hawatahudhuria

"Najua ni wengi mnanipenda na KuniSupport kwa hali na mali... Wote mnathamani kwangu na nilitamani kufanya jambo ambalo wote tungeweza kuhudhuria, lakini kwa siku ya kesho imeniladhimu kuwaalika wachache kisha hafla ya pamoja itafuata... kwa mtaokua majumbani mtaweza kushuhudia live kupitia Wasafi TV kuanzia saa moja ya Usiku," Diamond alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ingawa staa huyo wa Bongo hakutangaza kitakachofanyika usiku wa Jumatatu, wengi waafla hiyo na tetesi ambazo zimekuwa zikieenea kwamba anapanga kufunga pingu za maisha na kipenzi chake kipya.

Hivi majuzi Mama Dangote alifichua kwamba ni kweli ndoa ya mkeka ilifanyika na kutangaza mengi yangewekwa bayana Aprili 11.

"Ni kweli kulikuwa na ndoa ya mkeka. Tutazungumza zaidi Tarehe 11 Inshallah," Alisema.

Kupitia kwenye ukurasa wake aliandika;

"Panapo maajaliwa leo nitamtambulisha nimpendae,niliezama kwenye huba na kuridhia nae," Aliandika Diamond.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved