'Tutaambiwa watu nini,'Wanamitandao wawauliza Mulamwah na Sonie baada ya madai ya kurudiana

Muhtasari
  • Uvumi zaidi ulikuwa umejaza akaunti za mitandao ya kijamii huku pande zote mbili zikidai mwenzie alitapeliwa
  • Hivi majuzi, Mulamwah alidai kuwa mtoto huyo hakuzaa naye akimlaumu Carol kwa kulala na wanaume tofauti
Image: INSTAGRAM/CAROL SONNIE

Kwa mwonekano wa mambo, wanandoa mashuhuri Mulamwah na Sonie wako sawa.

Kupitia video iliyopakiwa kwenye ukurasa wa instaramwa Mulamwah, mcheshi huyo na Sonnie Carol wanaonekana kuwa katika mapenzi tena.

Unaweza kuita kutafuta kiki lakini inabakia kuwa ukweli kwamba wanandoa bado wako pamoja.

Video hiyo ilinakiliwa na maneno yaliyosomeka: "Keilah si mtoto wangu. Keilah ni mtoto wetu."

Mashabiki wameshangazwa na video hiyo iliyopakiwa kwa kuwa wengi wao waliamini kuwa wanandoa hao walikuwa wameachana.

Uvumi zaidi ulikuwa umejaza akaunti za mitandao ya kijamii huku pande zote mbili zikidai mwenzie alitapeliwa.

Hivi majuzi, Mulamwah alidai kuwa mtoto huyo hakuzaa naye akimlaumu Carol kwa kulala na wanaume tofauti.

Pia alikuwa amemshutumu kwa kujaribu kuavya mimba kwa mtoto huyo akiwa na miezi mitatu kutokana na kuchanganyikiwa kuhusu baba.

Mashabiki wao wanangoja kufahamu kama kuungana kwao ni kweli!

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

mpashogram: Sijuii tutaambia nini watu ๐Ÿ˜ฎ๐Ÿ˜ฎ

jalangoo: Mambo ni mengi....masaa ni chache..

djshiti_comedian: Munatufanya wambea tuonekane wabaya๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ

holydavemuthengi: Aii we canโ€™t keep up. ๐Ÿ˜ณ Hizi confusion zitafanya watu wakae single. ๐Ÿ˜’

murugi.munyi: Heh.. wait. You go off instagram for 2 minutes a couple has broken up, moved on, taken a dna test and gotten back together manze I canโ€™t keep up ๐Ÿคฃ