Binti wa mwisho kuzaliwa wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko, Sandra Mbuvi almaarufu Thicky Sandra alishirikisha wafuasi wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram.
Katika kipindi hicho, Sandra alizungumzia masuala kadhaa kuhusu maisha yake kama alivyoulizwa na wafuasi wake.
Kipusa huyo aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mchumba na hayupo katika harakati za kutafuta.
"Nipo single na sitafuti.. nataka muda wangu na sihitaji mwanaume," Sandra alijibu mashabiki waliouliza kuhusu hali ya mahusiano yake.
Sandra alipoulizwa kuhusu mipango yake ya siku za usoni aliweka wazi kwamba hana mipango ya kuwahi kupata watoto.
"Hapana" Sandra alijibu mfuasi aliyeuliza kuhusu mipango yake ya uzazi.
Mfanyibiashara huyo mdogo alisema ikiwa angetakiwa kuchagua kati ya pesa na furaha angependa kuishi kwa furaha badala ya utajiri.